Wazazi wapendwa,
Mtaa wa afia ya MITI-MURHESA inawajulisha ya kwamba, tangu siku ya ine tarehe 10 mwezi wa Kumi mpaka siku ya posho tarehe 12 mwezi wa Kumi 2024, itaundaliwa kipindi ya Tatu ya kampeni ya chanjo kwa kukinga watoto wa tangu kuzaliwa mpaka myaka tano na ugonjwa wa polio ama vunja vunja ndani ya mitaa yote ya afya 34 jimboni kivu ya kusini.
Tunawakumbusha ya kwamba kuna watoto wengi bado hawaja pata chanjo moja tangu kuzaliwa na wengine hawaheshimu kalendari ya chanjo ya kawaida.
Hali kama na hii inasababisha visa nyingi ya magonjwa ya watoto, kama vile vunja vunja yenyi ku ripotiwa mara kwa mara jimboni mwetu na kuleta ulemavu ata kuhatarisha maisha yao. Chanjo ni njia moja na bora ya kuepusha mtoto na iyi ugonjwa.
Ndio maana wahimizaji watapita mlango kwa mlango kutambuwa watoto wanao husika, na kuwajulisha wazazi kama wanganga watapita tangu siku ya ine tarehe 30 kuwapa chanjo zakuwakinga na polio nani bila malipo.
Chanjo ni haki ya mtoto, ni pashwa kwa mzazi na kwa serkali.
Imesahiniwa pa kavumu, tarehe 29/09/2024
Kwa niaba ya mtaa wa afia wa MITI-MURHESA
Dr Serge CIKURU MUNYAHU, Mganga mkuu wa afya pa Miti-Murhesa